Ban na Rais Mohamud wajadili ustawi na maendeleo Somalia

30 Januari 2015

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon, amesema kuwa Somalia inatakiwa kuweka ustawi wa kisiasa iwapo inataka kupiga hatua za maendeleo kufikia ndoto yake ya Vision 2016.

Ban amesema hayo alipokutana na rais wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud, pembezoni mwa mkutano wa viongozi wa Umoja wa Afrika, AU.

Bwana Ban amekaribisha ahadi ya Rais Mohamud za kufanya juhudi zote za kuunda serikali mpya kwa ushirikiano na bunge la Somalia.

Katika mkutano huo, wamejadili pia kuhusu haja ya kuunga mkono kampeni ya kijeshi ya pamoja ya kijeshi inayotekelezwa na jeshi la taifa la Somalia na vikosi vya Muungano wa Afrika, AMISOM, pamoja na haja ya mchakato jumuishi wa kuendeleza taifa.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter