Mjumbe Djinnit kukutana na washikadau wa maziwa makuu Adis Ababa

29 Januari 2015

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu ukanda wa Maziwa Makuu, Saïd Djinnit, amekutana na vikundi vya jamii wakati wa mdahalo wa mashauriano uliyoandaliwa na Shirika la msaada wa kibinadamu la Oxfam International na lile la Réseau pour la Réforme du Secteur de Sécurité et de Justice, RRSSJ pembezoni mwa Mkutano wa Umoja wa Afrika, AU  mjini Addis Ababa.

Mkutano huo unakuja miaka miwili baada ya kusainiwa kwa mkataba wa amani wa kihistoria ya Mfumo wa Amani, Usalama na Ushirikiano, PSCF, na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC na nchi 11 katika kanda.

Tukio hilo la kila mwaka huwaleta pamoja mashirika yasiyokuwa ya kiserikali kutoka ukanda ya Maziwa Makuu ili kushiriki moja kwa moja na Mjumbe Maalum kuhusiana na masuala ya kipaumbele kama vile amani, haki za binadamu na usalama.

Wakati wa mkutano wa leo, Bwana Djinnit amezungumza kuhusu changamoto ya utekelezaji kamili wa makubaliano amani, ulinzi na usalama huko DRC,  ikiwa ni pamoja kundi la FDLR kutoweka chini silaha kikamilifu, kuendelea kuwepo kwa makundi ya waasi mashariki mwa DRC, na maendeleo ya pole pole kuhusu urejeshaji makwao kwa wapiganaji  wa  zamani wa M23.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter