Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNDP na washirika kupambana na ukatili wa kijinisa Misri

UNDP na washirika kupambana na ukatili wa kijinisa Misri

Shirika la Umoja wa Mataifa la mpango wa maendelo UNDP,  Baraza la wanawake  NCW,  kwa kushirikiana na wizara ya sharia, mambo ya ndani na wizara ya mambo ya kigeni ya Misri , zimezindua mpango wa kupambana na ukatili dhidi ya wanawake.

Kwa mujibu wa taarifa ya shirika la UNDP mpango huo umezinduliwa mjini Cairo na kuhudhuriwa na wakuu wa UNDP na wizara  tajwa ambapo kwa amujibu wa utafiti wa Umoja wa Mataifa uliofanywa mwaka 2013, asilimia 99 ya wanawake nchini Misri, wamekutana na unyanysaji wa kijinsia.

 Mpango huu unalenga kutataua tatizo hili kwa kuimarisha uwezo wa taasisi za serikali na vyombo vyake pamoja na kutoa taarifa kwa umma kuhusu madhara ya unyanyasaji dhidi ya wanawake na wasichana, familia na jamii kwa ujumla. Kadhalika mpango huu utawajumuisha wananchi kwa kuunganisha taarifa za hatua za kisheria kwa kupitia njia za kiteknolojia.

Mkuu wa UNDP nchini Misri Ignacio Artaza amesema ukatili dhidi ya wanawake na wasichana ni kosa ambalo halifai kuvumilika na kuwaacha watekelezaji wa ukatili huu huru. Ameongeza kuwa ukomeshwaji wa ukatili huo ni muhimu kwani ni haki ya msingi isiyo na kificho.

 Mradi unafadhiliwa na UNDP na utawezesha maafisa wa Misri kutekeleza vyema na kusaidia juhudi hizi katika nchi nzima ili kutatua tatizo hilo