Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNFIL yamuaga mlinda amani wake aliyeuawa

UNFIL yamuaga mlinda amani wake aliyeuawa

Huko Lebanon hii leo kwenye uwanja wa ndege wa Beirut kumefanyika ibada ya kuaga mwili wa mlinda amani wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini humo, UNFIL aliyeuwa jana akiwa lindoni.

Mlinda amani huyo Francisco Javier Soria Toledo kutoka Hispani aliuawa wakati wa mapigano makali kwenye eneo la amani lililo mpakani mwa Lebanon na Israel.

Hadi sasa chanzo cha kuuawa kwake hakijafahamika na kinafanyiwa uchunguzi.

Mkuu wa ujumbe wa UNFIL ambaye pia ni Kamanda mkuu Meja Jenerali Luciano Portolano ametuma rambirambi zake kwa familia ya mlinda amani huyo na serikali ya Hispania akisema tukio hilo linadhihirisha vile ambavyo wanaotekeleza majukumu adhimu ya Umoja wa Mataifa wanavyokabiliwa  na mazingira magumu.