Serikali ya Somalia ipongezwe kwa juhudi za kuendeleza haki za watoto- Nyanduga

29 Januari 2015

Mtalaam huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watoto nchini Somalia, Tom Bahame Nyanduga, amesema serikali ya Somalia inapaswa kupongezwa kwa jitihada zake katika kuendeleza haki za watoto.

Ameeleza kwamba kuridhiwa kwa Mkataba wa haki za watoto ni dalili inayoonyesha kwamba serikali inajitahidi kukabiliana na changamoto kadhaa zinazoikumba nchi, mathalan tatizo la njaa lililoathiri nchi hiyo mwaka uliopita.

Mtalaam huyo amesema juhudi zinazofanyika katika kurejesha hali ya usalama nchini humo kwa ushirikiano na jumuiya ya kimataifa ni muhimu sana ili nchi iweze kutekeleza miradi ya maendeleo, hasa kwa ajili ya elimu na afya ya watoto, ambavyo ni misingi ya haki yao.

(Sauti ya Nyanduga)

Awali mwezi wa Januari, bunge la Somalia limeridhia mkataba wa haki za watoto, Somalia ikiwa ni nchi ya 194 kuridhia mkataba huo.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter