Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kamati ya haki za wabunge yaangazia bara la Asia

Kamati ya haki za wabunge yaangazia bara la Asia

Mkutano wa siku nne wa kamati ya haki za binadamu kwa wabunge umefikia tamati huku ukipitisha  maamuzi muhimu yanayogusa maeneo mbali mbali duniani.

Taarifa ya umoja wa mabunge duniani, IPU imetaja maamuzi hayo yamegusia mathalani Sri Lanka ambapo wajumbe wamesema ni matumaini yao kuwa serikali itachukua hatua muhimu kuwafiisha mbele ya sheria watuhumiwa wa mauaji ya wabunge wawili ya mwaka 2005 na 2006.

Wamesema ni matumaini yao kuwa madai ya kuhusika kwa serikali na wanamgambo kwenye mauaji hayo ni vyema yachunguzwe na matokeo yawekwe hadharani.

Kamati hiyo ilipitia hali ya wabunge 301 kutoka mataifa 40 na kueleza wasiwasi wake kuhusu hali ya Malaysia ambako wakili wa kiongozi wa upinzani Anwar Ibrahim anakabiliwa na mashtaka ya fitna wakati hukumu ya kesi ya pili ya ulawiti inayomkabili mteja wake ikitarajiwa kutolewa mwezi ujao.

Wakati wa kikao hicho, mbunge wa Uingereza Ann Clwyd amechaguliwa kuwa Rais wa kamati hiyo baada ya Seneta Juan Pablo Letelier kumaliza muda wake.