Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maazimio kuhusu Syria yanapuuzwa: OCHA

Maazimio kuhusu Syria yanapuuzwa: OCHA

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa leo limepata ripoti kuhusu hali ya kibinadamu nchini Syria ambapo ofisi ya umoja huo inayoratibu masuala ya kibinadamu, OCHA imesema hali inazidi kuwa mbaya na hata kuwafikia wahitaji ni taabu huku maazimio yakipuuzwa. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Mzozo wa Syria ukiingia mwaka wa Tano, utekelezaji wa maazimio ya Baraza la Usalama umeendelea kugonga mwamba ikiwemo matumizi ya silaha kwenye makazi ya watu kunakofanywa na serikali na waasi.

Huo ni ujumbe wa Naibu Mkurugenzi wa wa OCHA Kyung-wha Kang kwa wajumbe wa Baraza hilo akisema hali inazorota kila uchao..

(Sauti ya Kyung-Wa)

“Shule na hospitali hazijaachwa kwenye mashambulio hayo. Madaktari wa haki za binadamu wameripoti mashambulizi manane kweney vituo vya afya mwezi Disemba, takriabni shule tatu ziliripotiwa kutunguliwa na makombora ya serikali mwezi Disemba na kuua watoto Tisa na kujeruhi wengine wengi."

Amesema hali inatia hofu zaidi kwenye majimbo ya Raqqa na Derazur yaliyo chini ya kikundi cha ISIL kwa kuwa...

(Sauti ya Kyung-Wa)

“Mashirika ya Umoja wa Mataifa yalishindwa kuwasilisha misaada kwa watu 600,000 kwenye majimbo hayo mawili  mwezi DIsemba kutokana na kutokuwepo kwa makubaliano na vikundi vilivyojihami kwenye maeneo hayo.”