Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zeid alaani mauaji ya watu 20 Misri

Zeid alaani mauaji ya watu 20 Misri

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein ameelezea kusikitishwa kwake na vifo vya watu 20 wakati wa mapambano kati ya waandamanaji na vikosi vya usalama nchini Misri ijumaa.

Akiongea mjini Geneva Kamishna Zeid ameitaka mamlaka za Misri kuchukua hatua za dharura kukomesha matumizi ya nguvu za ziada yanayofanywa na vikosi vya usalama. Rupert Colville ni msemaji wa ofisi ya haki za binadamu

(SAUTI RUPERT)

Kamishina mkuu amesema kuwa utulivu wa kudumu nchini Misri utawezekana tu ikiwa haki za msingi zitaheshimiwa, vinginevyo huzuni na hisia za watu za kutotendewa haki zitaongezeka na kukuza machafuko ya kijamii na kisiasa. Ameelezea shauku yake kwa makundi yote kujihusiha katika mazungumzo na kupatia suluhisho la matatizo ya Misri.”

Watu hao waliouwawa akiwemo mwanaharakati mwanamke Shaimaa Al Sabagh, yalifanyika katika maeneo tofauti mjini Alexandria na Cairo wakati wa maandamano ya maadhimisho ya mandamano ya mapinduzi ya mwaka 2011 yaliyomuondoa madarakani Rais wa wakati huo Hosni Mubarak ambapo taarifa zinasema watu wengine zaidi ya 90 walijeruhiwa.