Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Watoto Ukraine walazimika kuishi makazi ya kuzuia bomu- UNICEF

Watoto Ukraine walazimika kuishi makazi ya kuzuia bomu- UNICEF

Mapigano yanayoendelea nchini Ukraine yamewalazimu watoto wapatao 1,000 na familia zao kuhamia kwenye makazi ya kuwalinda kutokana na mabomu kwenye mji wa Donetsk, mashariki mwa nchi, limesema shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF.UNICEF imesema kuna hatari kubwa kiafya ya kuzuka magonjwa kama vile ule wa kupooza, yaani polio, kwa watoto nchini humo. Imetoa wito mapigano yasitishwe mara moja kati ya vikosi vya serikali na waasi, na kwa pande zote kuhakikisha usalama wa watoto. Giovana Barberis ni mwakilishi wa UNICEF nchini Ukraine

Watoto huumia kisaikolojia, wanashindwa kwenda shule na wamo hatarini kuambukizwa magonjwa tofauti kwa sababu hakuna usafi na dawa za chanjo.”

Kwa mujibu wa UNICEF, watoto milioni 1.2 wameathiriwa na mzozo wa Ukraine, na cha kutia hofu zaidi ni hatari ya kuzuka mlipuko wa polio kwani watoto wapatao milioni 1.5 chini ya umro wa miaka mitano hawajapewa chanjo dhidi ya polio.