Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNRWA kutoa tamko kuhusu ujenzi mpya wa Pwani ya Gaza

UNRWA kutoa tamko kuhusu ujenzi mpya wa Pwani ya Gaza

Shirika la Umoja wa Mataifa la  kusaidia wakimbizi wa Palestina URNWA, leo litatangaza msimamo kamilifu kuhusu ujenzi mpya wa pwani ya ukanda wa Gaza.

Kwa mujibu wa afisa habari wa UNRWA Adnan Abu Hasna,  tangazo hilo litatokana na kikao mjini Jerusalem  baina ya maafisa wa UNRWA na wawakilishi wa nchi  wahisani kikao kinachojadili maendeleo ya ujenzi upya wa eneo hilo.

UNRWA mara kwa mara imekuwa ikilalamikia upungufu wa fedha inazopokea kutoka kwa nchi wahisani kwa ajili ya ujenzi wa ukadna wa pwanai ya Gaza hatua ambayo husababisha ucheleweshaji wa mipango ya  ujnezi mpya wa eneo hilo.