Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Bila usalama wa chakula hakuna amani: FAO

Bila usalama wa chakula hakuna amani: FAO

Mkurugenzi Mkuu wa shirika la chakuala na kilimo, FAO, Graziano da Silva amesema amani haiwezi kufikiwa duniani ikiwa hakuna usalama wa chakula akisisitiza kuwa njaa ndiyo inayoongoza kwa kuuwa watu wengi duniani na sio vita.

Katika mahojianoa na radio ya Umoja wa Mataifa da Silva amesema harakati za kutoa msaada wa chakula wakati wa majanga mathalani vita sio suluhisho mujarabu la vita na akaenda mbali zaidi na kusema

(Sauti ya Graziano)

"Na katika hili watoto ndiyo waathirika wakuu,  na mama ndiye mwenye jukumu la kulisha familia na jukumu hili linaanza tangu mwanzo. Tunachokiona ni kwamba hili huvunja familia."

Mkuu huyo wa FAO ni miongoni mwa wazungumzaji katika mkutano kuhusu usalama wa chakula na amani na juhudi za ujenzi mpya baada ya kadhia ya Ebola.