Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwajibikaji ni muhimu katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu: wataalam wa UM

Uwajibikaji ni muhimu katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu: wataalam wa UM

Wataalamu maalum wa Haki za Binadamu katika Umoja wa Mataifa wamesisitiza kuwa malengo endelevu ya baada ya mwaka 2015 yanayojadiliwa na jamii ya kimataifa ni lazima yajikite katika misingi imara ya viwango vya kimataifa vya haki za kibinadamu pamoja na kuhakikisha uwajibikaji katika kutimiza malengo hayo. Taarifa zaidi na Abdullahi Boru

(Taarifa ya Abdullahi)

Wito wa wataalamu hao ulitolewa wakati ambapo nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa wameaza majadiliano ya kukamilisha rasimu ya malengo ya maendeleo endelevu 17, SDGs ambayo yatakuwa nguzo maalum ya ajenda na sera ya maendeleo ya kimataifa kwa zaidi ya miaka 15 ijayo.

Malengo hayo ya maendeleo yatajadiliwa na kupitishwa wakati wa mkutano wa wakuu wa nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa utakaofanyika New York mwezi Septemba mwaka 2015.

Katika taarifa, wataalamu hao wamesema wanakaribisha mkazo unaowekewa utekelezaji na uwajibikaji, na kwa hiyo wamesisitiza upigiwe chepuo zaidi.

Mojawapo ya mapendekezo halisi ya wataalamu hao ni pamoja na kuimarisha kumbukumbu ya kulinda uhuru wa kimsingi  wa kujieleza, uhuru wa kujiunga na chama sawa na kushiriki mkutano wa amani.