Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ebola ni janga lililotoa mafunzo-WHO

Ebola ni janga lililotoa mafunzo-WHO

Ugonjwa wa homa kali ya Ebola ni janga ambalo limelioa masomo  kwa shirika la afya ulimwenguni (WHO) kuhusu namna ya kuzuia matukio kama hayo wakati ujao.

Hii ni kwa mujibu wa wa Mkurugenzi mkuu wa WHO Margaret Chan, wakati akizungumza kwenye kikao maalum cha bodi ya shirika hilo cha kutathimini makabiliano dhidi ya kirusi cha  Ebola mwishoni mwa juma.

Mlipuko wa Ebola umezikumba zaidi nchi za Afrika magharibi ambazo ni Guinea, Liberia na Sierra Leone ambapo zaidi ya watu 8000 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa huo.

Bi Chan amesema WHO ilisaidia kuanzisha maabara, kusimamia ujenzi wa matibabu ya Ebola, na kuratibu kupeleka kwa vikundi vya matatabibu takribani 60 na hivi karibuni WHO imepeleka wafanyakazi 700 katika nchi tatu zilizoathiriwa zaidi. Hata hivyo amesema..

Hata hivyo Mkurugenzi huyo amesema mlipuko wa Ebola umeleta haja ya mabadiliko ya dharura katika maeneo mengi ikiwamo namna WHO inavyofanya kazi wakati wa dharura.

Mlipuko wa Ebola umebainisha baadhi ya mapungufu katika utawala wa shirika, menejimenti, na miundombinu ya kiufundi.

Kufuatia hilo Bi Chan amependekeza mabadiliko kadhaa kama vile kutengeneza taratibu za ajira na kuongezea uwezo zaidi kwa sheria za kimataifa za afya. Amesema kuhusu uzalishaji zaidi wa dawa,  dunia lazima isijikute mikono mitupu janga kama la Ebola likiibuka.