Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNSMIL walaani shambulio katika ofisi za UNDP Libya

UNSMIL walaani shambulio katika ofisi za UNDP Libya

Umoja wa Mataifa umelaani shambulio  lililotekelezwa na watu wasiofahamika waliojihami kwa silaha nje ya ofisi ya Umoja huo ya mpango wa maendeleo kitaifa UNDP mjini Tripoli, Libya.

Taarifa iliyotolewa na mkuu wa  Ujumbe wa Umoja wa Mataifa chini Libya UNSMIL Bernardino Leon imesema washambuliaji hao walikuwa katika gari ambalo halikusimama baada ya kuwashambulia askari waliokuwa zamu nje ya ofisi za UNDP.

Hakuna wafanyakazi wa UM waliohusishwa katika shambulio.

UNSMIL inasema askari wa kidiplomasia wanachunguza tukio hilo kufahamu kisa chake.

UNSMIL katika taarifa yake imetuma salamu za rambirambi kwa askari walioshambuliwa na kutaka askari kuhusika kikamilifu katika uchunguzi.