Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Katibu Mkuu asihi pande zote nchini Yemen kujizuia na kudumisha amani

Katibu Mkuu asihi pande zote nchini Yemen kujizuia na kudumisha amani

Katibu Mkuu Wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki-moon ana wasiwasi mkubwa kuhusu hali nchini Yemen, ambapo Rais Abd Rabbo Mansour Hadi na Waziri Mkuu Khaled Bahah wamejiuzulu mapema leo.

Katika taarifa, Bw Ban ametoa wito kwa pande zote wakati huu ambapo hali ni tete kujizuia na kudumisha amani na utulivu.

Halikadhalika, Katibu Mkuu ametaka pande zote kushirikiana kikamilifu na Mshauri wake Maalum kuhusu Yemen, Jamal Benomar, ambaye yuko mjini Sana'a na anashauriana kwa ukaribu na pande zote katika kusaidia upatikanaji wa suluhu kwa mgogoro wa sasa nchini.