Ushiriki wa jamii msingi wa vita dhidi ya umaskini Tanzania

23 Januari 2015

Wakati Malengo ya Maendeleo ya Milenia yanafikia ukomo mwaka huu, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameanzisha kampeni ya kuelimisha jamii na kushawishi wadau wote ili kuchukua hatua katika kutokomeza umaskini.

Kongamano la kimataifa litakalofanyika mjini New York mwezi Septemba mwaka 2015 linatakiwa kubaini malengo mapya yatakayoongoza shughuli za kupambana na umaskini duniani kwa kipindi cha miaka 15 ijayo.

Mashirika yasiyo yakiserikali yameshiriki katika uzinduzi wa kampeni hiyo, ikiwemo mtandao wa kampeni ya kuondoa umaskini Tanzania, ambayo imeongoza tukio maalum, mjini Dar es Salaam, siku chache zilizopita.

Mratibu wa mtandao huo, Finland Bernard, ameiambia Redio ya Umoja wa Mataifa kwamba ushiriki wa jamii na asasi zisizo za serikali ni muhimu sana katika kufikia malengo ya kutokomeza umaskini. Katika mahojiano na Priscilla Lecomte, ameanza kwa kueleza mafanikio ya Tanzania katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo ya milenia.

(Sauti ya Bernard)

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter