Harakati za kujikwamua na mimba za utotoni Uganda

Harakati za kujikwamua na mimba za utotoni Uganda

Ripoti ya Shirika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa, UNFPA inasema kuwa  Kila mwaka, wasichana Milioni 7.3 wenye umri usiozidi miaka 18 hupata ujauzito na kujifungua. Ripoti hiyo kuhusu hali ya idadi ya watu mwaka 2013, imesema, milioni mbili kati yao hao ni watoto wenye umri usiozidi miaka 14, na kwamba watoto hao hukumbana na matatizo ya muda mrefu ya kiafya na kijamii kutokana na mimba hizo bila kusahau vifo wakati wa kujifungua.

Pamoja na ripoti hiyo kutoa wito wa kubuni mbinu za kina za kukabiliana na changamoto za mimba za utotoni, pia inahimiza uwekezaji zaidi katika elimu ili kuhakikisha watoto wa kike wanaendelea kuwa shuleni, kutokomeza ndoa za utotoni, kubadilisha mitazamo kuhusu majukumu ya kijinsia na usawa wa kijinsia. Pia inapendekeza kuongeza ufikishaji wa huduma za afya ya uzazi kwa watoto walobalehe, zikiwemo kuzuia mimba na kuboresha usaidizi kwa wazazi wa utotoni.

Je hali ikoje katika ukanda wa Afrika Mashariki na wadau wanasemaje kuhusu utokomezwaji wa ndoa hizo kwa kutumia mbinu mbadala? Ungana na John Kibego kutoka Hoima nchini Uganda.