Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban afanya mazungumzo kwa simu na mfalme Mohammed VI wa Morocco

Ban afanya mazungumzo kwa simu na mfalme Mohammed VI wa Morocco

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban ki-Moon amefanya mazungumzo kwa njia ya simu na mfalme wa Morocco Mohammed VI alhamisi wiki hii ambapo Ban ameelezea shukrani zake kwa mchango wa thamani wa nchi hiyo katika shughuli mbalimbali za Umoja wa Mataifa hususani katika ulinzi wa amani na masuala mengine muhimu barani Afrika na Mashariki ya Mbali.

Kwa mujibu wa taarifa ya msemaji wa Katibu mkuu, Ban pia amemshukuru mfalme Mohammed VI kwa ushiriki wan chi yake katika majadiliano yanayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa, baina ya ufalme wa Morocco na kundi la  Frente Polisario na kuongeza kuwa taarifa itakayotolewa kwa baraza la usalama juu ya majadiliano hayo itaakisi ukweli.

Pia Ban amesisitiza kuwa ujumbe wa Umoja wa Mataifa magahribi mwa jangwa la Sahara MINURSO, utaendelea kutekeleza majukumu yake kwa mujibu wa mamlaka ya baraza la usalama

Kwa upande wake mfalme wa Morocco amesema anatarajia uhusiano baina ya nchi yake na Umoja wa Mataifa utakuzwa na kwamba mwakilishi wa Morocco katika Umoja huo ataendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu katika MINURSO ili kuandaa ziara ya Ban nchini humo haraka iwezekanavyo.