Ban akaribisha makubaliano ya SPLM huko Arusha

23 Januari 2015

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amekaribisha makubaliano baina ya pande kinzani kwenye chama cha People’s Liberation Movement, SPLM ambayo yametiwa saini huko Arusha Tanzania tarehe 21 mwezi huu.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Stephan Dujarric ametoa wito kwa utekelezaji wa haraka wa makubaliano hayo hususan Rais Salva Kiir na Dkt Riek Machar kuazimia tena kuwa wanaheshimu mkataba kusitisha chuki na kuhamisha pande zote zilizotia saini kupatia suluhu suala la uongozi ndani ya chama hicho.

(Sauti ya Stephan)

Katibu mkuu anakumbusha pande zote kuwa muda unayoyoma. Amewasihi kutumia fursa ya mkutano ujao wa viongozi wa IGAD kufikia makubaliano ya kumaliza mgogoro, ikiwemo kanuni ya kuwa na serikali ya pamoja na hatua za kushughulikia chanzo cha mzozo na kuhakikisha uwajibikaji.”

Makubaliano hayo ya Arusha yaliratibiwa na chama tawala nchini Tanzania, CCM chini ya mwenyekiti wake Rais Jakaya Kikwete.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter