Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maendeleo ni lazima yajumuishe wanawake na kulinda mazingira- Kagame

Maendeleo ni lazima yajumuishe wanawake na kulinda mazingira- Kagame

Rais Paul Kagame wa Rwanda amesema leo kuwa kufanya maendeleo si suala la chaguo kati ya mazingira na ukuaji, bali ni suala la kufikiria jinsi ya viwili hivyo vinaweza kwenda sambamba, kwani vinategemeana.

Rais Kagame amesema hayo kwenye jukwaa la kimataifa kuhusu uchumi huo Davos, Uswisi, akiongeza kuwa nchini Rwanda, masuala ya maendeleo na kulinda mazingira yanazingatiwa kwa njia jumuishi nay a kuendeleza usawa, akisisitiza haja ya kujumuisha wanawake.

“Wanawake, kwa mfano nchini Rwanda, ni asilimia 52. Kwa hiyo ukiwaacha asilimia 52 ya watu nje ya shughuli za kiuchumi, unakuwa huna akili.”

Rais Kagame amesema inawezekana kuzalisha zaidi na wakati huo huo, kulinda mazingira..

“Inaeleweka duniani na hata nchini Rwanda kuwa kuna haja ya kuzalisha zaidi na haja ya matumizi zaidi, lakini ni lazima kufanya hivyo kwa njia endelevu, na huwezi kufanya hivyo kwa njia endelevu bila kuzingatia jinsi unavyofanya maendeleo na wakati huo huo kulinda mazingira.”