Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Twachoshwa na madai kuwa hatulindi mashahidi: Kenya

Twachoshwa na madai kuwa hatulindi mashahidi: Kenya

Serikali ya Kenya na msajili wa mahakama ya kimataifa ya makosa ya uhalifu, ICC  huko The Hague, wanaendelea na mashauriano ya kuwezesha nchi hiyo kuendelea kupatiwa orodha ya mashahidi ili waweze kuwapatia ulinzi.

Kauli hiyo imetolewa na Mwanasheria Mkuu wa Kenya Githu Muigai alipozungumza na waandishi wa habari mjini Geneva ambao walidai kuwepo kwa vitisho dhidi ya mashahidi wanaotakiwa kwenye kesi inayoendelea The Hague.

(Sauti ya Githui)

“Mambo yanayokatisha tamaa zaidi serikali ni haya madai kurejewa mara kwa mara kwamba Mosi hamuwapatii ulinzi mashahidi lakini tunafahamu kuwa hamufahamu mashahidi na hatuwezi kuwapatia majina yao lakini bado mnatakiwa muwalinde.”

Bwana Muigai amesema kimsingi orodha ya mashahidi hupatiwa upande wa mashtaka na utetezi lakini wiki mbili zilizopita walipatiwa orodha ya mashahidi na imeleta mafanikio.

(Sauti ya Githui-)

“Pindi tunapopatiwa orodha ya mashahidi kama ilivyofanywa hivi karibuni tumeweza kuchukua haraka na tukaweza kuwapatia ulinzi wetu.”

Mwanasheria huyo Mkuu wa Kenya akasema..

(Sauti ya Githui-)

“Hatimaye mahakamaka imebaini kuwa ni lazima itupatie orodha ya majina ya mashahidi ambayo itataka tuwapatie ulinzi.”