Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNSMIL yalaani shambulizi la silaha kwenye Benki Kuu ya Libya, Benghazi

UNSMIL yalaani shambulizi la silaha kwenye Benki Kuu ya Libya, Benghazi

Ujumbe wa Umoja Mataifa nchini Libya, UNSMIl, umelaani shambulizi lililoripotiwa kutekelezwa dhidi ya Benki Kuu ya Libya tawi la Benghazi, ambayo imetajwa kuwa taasisi muhimu ya taifa la Libya.

UNSMIL imesema, inaamini kuwa kuwekwa kwa tume ya uchunguzi kutasaidia kubainisha ni nini hasa kilichofanyika, huku ikitoa wito kwa pande zote nchini Libya kushirikiana na tume hiyo, Benki Kuu ya Libya na vyombo vya sheria.

Ujumbe huo umesema tukio hilo na kukiukwa kwa makubaliano ya kusitisha mapigano hivi karibuni kunaonyesha haja ya kuongeza kasi ya kuendeleza mchakato wa mazungumzo ya amani.

UNSMIL imezitolea wito pande zote kuendelea kushiriki mchakato huo, ambao unalenga kurejesha amani na utulivu nchini Libvya, zikiweka maslahi ya taifa mbele ya mengine yote.