Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Naibu Mwakilishi wa UM Somalia awasili Mogadishu kusaidia ujenzi wa amani na taifa

Naibu Mwakilishi wa UM Somalia awasili Mogadishu kusaidia ujenzi wa amani na taifa

Naibu mpya wa Mwakilishi maalum wa Katibu Mkuu nchini Somalia, Raisedon Zenenga, amewasili mjini Mogadishu hii leo kuanza majukumu yake kwenye Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Somalia, UNSOM.

Kama sehemu ya wajibu wa UNSOM, Bwana Zenenga atajikita kwenye kuunga mkono Somalia katika masuala ya kipaumbele kisiasa, utawala wa sheria na taasisi za usalama.

Bwana Zenenga ameelezea kufurahia fursa aliyopewa kurejea Somalia ili kuunga mkono jitihada za watu wa Somalia kutimiza ndoto zao za kuwa na mustakhbali wenye amani, utulivu na maendeleo. Amesema changamoto ni nyingi, lakini ni sharti kufanya kazi pamoja ili kusukuma mbele maendeleo ambayo watu wa Somalia wanataka kuona.