Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF yampongeza Angelique Kidjo kwa tuzo aliyepewa Davos

UNICEF yampongeza Angelique Kidjo kwa tuzo aliyepewa Davos

Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto, UNICEF, limempongeza mwimbaji wa Benin Angelique Kidjo kwa kushinda tuzo la Crystal Award, linalotambua wasaani kwa kipaji chao lakini pia kwa juhudi zao katika kubadili dunia.

Angelique Kidjo, ambaye ni Balozi mwema wa UNICEF kuhusu elimu kwa wasichana tangu mwaka 2002, amepewa tuzo hilo wakati wa uzinduzi wa kongamano la dunia kuhusu uchumi, huko Davos, Uswisi.

UNICEF imesema kwamba maamuzi ya kongamano la Davos kumchagua Bi Kidjo yanatambua siyo tu kipaji chake cha juu katika usanii, bali pia juhudi zake katika maswala ya kibinadamu.