Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kay alaani machafuko na kuhimiza utulivu Defow, kati mwa Somalia

Kay alaani machafuko na kuhimiza utulivu Defow, kati mwa Somalia

Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu na Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa Somalia, UNSOM, Nicholas Kay, amelaani machafuko ya hivi karibuni huko Defow, kati mwa Somalia, ambayo yameripotiwa kusababisha vifo vya watu kadhaa, wakiwemo wanawake na watoto.

Kay ametoa wito utulivu urejeshwe, akisisitiza haja ya kutatua mizozozano kwa njia ya mazungumzo ya amani na makubaliano.

Ameomba pande zote zijiepushe na machafuko na kuheshimu mchango wa wazee katika kutafuta suluhu la amani kwa mzozo uliopo. Kay pia amepeleka rambi rambi zake kwa familia za waathiriwa wa machafuko hayo ya hivi karibuni.