Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Misaada yawasili Al Waer, mji wa Homs

Misaada yawasili Al Waer, mji wa Homs

Kwa kushirikiana na Shirika la Hilali Nyekundu la Syria, Umoja wa Mataifa umefikisha malori kumi ya misaada kwa wakazi 75,000 wa mtaa wa Al Wa’er, kwenye mji wa Homs hapo jana.

Malori ya kwanza ya msafara huo yaliwasili kwenye mtaa huo mnamo tarehe 15 na 18 Januari.

Pamoja na misaada mingine iliyopangwa, msaada wa maziwa ya watoto ulifikishwa hapo jana, kulingana na tathmini iliyofanywa mnamo Januari 15, 2015. Umoja wa Mataifa haujaweza kufikisha misaada Al Wa’er tangu mwanzoni mwa Novemba mwaka uliopita, 2014.