Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Chupa za plastiki zisizooza zaleta nuru kwa wakazi huko Ufilipino.

Chupa za plastiki zisizooza zaleta nuru kwa wakazi huko Ufilipino.

Kitendo cha kuwasha taa kwa kubofya tu kiwashio ni jambo ambalo linaonekana ni la kawaida sana kwa baadhi ya watu. Hata hivyo kwa Moja ya Tano ya wakazi wa dunia, matumizi ya taa siyo jambo la kuchagua kwani kwao ni ndoto na hivyo ni maskini wa nishati hiyo ya mwanga. Mathalani nchini Ufilipino, kwa wananchi wanaoishi makazi duni kupata mwanga ni ndoto na kutokana na ujenzi wa makazi yao, giza huwepo hata mchana. Lakini sasa nuru imeingia na ndoto yao sasa imetimia kama ilivyo lengo la mwaka huu wa 2015 ambao umetajwa kuwa mwaka wa mwanga ili kuleta nuru na hatimaye kubadili maisha. Nini kimefanyika? Basi ungana na Assumpta Masso kwenye makala hii.