Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ghana yatokomeza Guinea Worm: WHO

Ghana yatokomeza Guinea Worm: WHO

Ghana imetangazwa rasmi kuwa haina tena ugonjwa wa minyoo ambao hufahamika kwa Kingereza Guinea Worm . Taarifa zaidi na Grace Kaneiya.

(TAARIFA YA GRACE KANEIYA)

Uamuzi uliofikiwa na shirika la afya ulimwenguni (WHO) unafuatia mapendekezo ya tume ya kimataifa ya kuthibitisha ukomeshwaji wa ugonjwa huo ambapo katika mkutano wake uliofanyika January 14- 15 mwaka huu kwa kauli moja ilipitisha kuwa hakuna maambukizi nchini Ghana.

Kwa mujibu wa WHO ni nchi nne pekee barani Afrika ikiwamo Chad, Ethiopia, Mali and South Sudan zenye visa vya ugonjwa huo.

Mwaka 2014 visa 126 viliripotiwa WHO ikilinganishwa na visa 148 mwaka 2013.