Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Vita dhidi ya baa la Nzige Madagascar mashakani: FAO

Vita dhidi ya baa la Nzige Madagascar mashakani: FAO

Shirika la chakula na kilimo duniani, FAO linahitajia nyongeza ya zaidi ya dola Milioni 10 nukta Tano ili kuepusha kuibuka tena kwa baa la nzige nchini Madagascar.

FAO imesema iwapo fedha hizo hazitapatikana ili kukamilisha mpango wake wa pamoja na serikali wa wa kutokomeza nzige, usalama wa chakula kwa watu Milioni 13 Madagascar utakuwa mashakani.

Annie Monard mratibu wa FAO kuhusu harakati dhidi ya nzige amesema ni muhimu wapate fedha hizo sasa kwani msimu wa mvua unakaribia na ndio kipindi cha mvua cha kuzaliana na hivyo fedha zitasaidia ununuzi wa vifaa kama dawa za kupulizia na mafunzo kwa wataalamu kuwa..

(Sauti ya Annie)

“Tulifanikiwa na tulisitisha baa hilo la nzige kwani waliweza kusukumwa hadi maeneo ya kusini ambayo ni maeneo yao asilia. Lakini sasa tunapaswa kuwa na uhakika kuwa aina zote za nzige wako katika kiwango cha chini zaidi na hawana uwezo wa kuzaliana tena haraka na kuibua baa lingine.”

Tayari FAO imeshatumia dola Milioni 28.8 kukabiliana na nzige ambao tangu mwaka 2012 wamekuwa tishio maeneo yote ya Madagascar.