Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wakimbizi wa Syria wapambana na baridi na theluji.

Wakimbizi wa Syria wapambana na baridi na theluji.

Zaidi ya wakimbizi Milioni moja kutoka Syria wametafuta hifadhi nchini Lebanon. Wengi wao wanaishi kwenye kambi za wakimbizi zinazosimamiwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia wakimbizi, UNHCR. Awali mwezi huu, dhoruba ya baridi kali ya kihistoria imepiga kambi ya wakimbizi iliyoko bonde la Bekaa.

Mahema yamejaa theluji na wakimbizi wanakabiliana na baridi kali zaidi. Wanawake na watoto wako hatarini kuathirika na magonjwa mbalimbali. UNHCR inawapelekea misaada maalum ili kujikinga na baridi hiyo.

Je hali iko vipi zaidi? Jiunge na Priscilla Lecomte kwenye makala hii.