Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Davos iibuke na mbinu bunifu za kutokomeza njaa duniani: WFP

Davos iibuke na mbinu bunifu za kutokomeza njaa duniani: WFP

Wakati kongamano la dunia kuhusu uchumi likitarajiwa kung’oa nanga siku ya Jumatano huko Davos Uswisi, Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP limesema kampuni zinapaswa kutambua uhusiano mkubwa uliopo kati ya kumaliza njaa na mafanikio ya kiuchumi na kibiashara.

Mkurugenzi Mkuu wa WFP Etharin Cousin katika taarifa yake amesema licha ya uhusiano huo bado hakuna hatua za dhati zinazochukuliwa kuhakikisha lengo la kutokomeza kabisa njaa duniani linafikiwa.

Amenukuu tafiti zinazoonyesha kuwa kila dola moja inayowekezwa katika lishe bora inaweza kuleta faida ya dola 166 katika biashara akisema ni vigumu kupata faida zaidi ya hiyo kwa kuwa inakwenda kwenye kuokoa maisha na kujenga jamii endelevu.

Kwa mantiki hiyo Cousin amesema watatumia mkutano huo kushinikiza wafanyabiashara kuwekeza kwenye mipango ya kuokoa maisha kama vile kuibuka na mbinu bunifu za kufikia lengo la kutokomeza njaa duniani.

Amesema kwa WFP tayari ina mipango ya kusaidia wakulima wadogo wadogo kupeleka mazao yao kwenye masoko mapya.