Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tume ya UM kuhusu mzozo wa Gaza wa 2014 yazuru Amman

Tume ya UM kuhusu mzozo wa Gaza wa 2014 yazuru Amman

Tume huru ya Umoja wa Mataifa kuhusu mzozo wa Gaza wa mwaka 2014, imefanya ziara mjini Amman, Jordan, ambako imefanya mikutanao ya faragha na mashahidi kadhaa kutoka ukanda huo.

Katika kutekeleza majukumu yao, wanachama wa tume hiyo tayari wamezungumza na mashahidi na wahanga kwenye Ukanda wa Gaza, Ukingo wa Magharibi, Jerusalem Mashariki, pamoja na Israel, na wanatarajia kusikia ushahidi zaidi katika wiki zijazo.

Wanatume hiyo wamesema wapo tayari kusafiri ili wakutane na mashahidi ana kwa ana iwapo serikali ya Israel itawaruhusu kufanya hivyo, au hali ya usalama ikiwaruhusu kuvuka kutoka Misri kwenda Ukanda wa Gaza.

Wanatume hao wamewashukuru waathiriwa na mashahidi ambao waliwaamini wakati wa ziara yao hiyo ya pili Amman, wakihadithia visa vya uchungu waliokumbana nao katika mzozo wa Gaza wa 2014.