Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yawakwamua waathirika wa mafuriko Malawi

WFP yawakwamua waathirika wa mafuriko Malawi

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP, kwa kushirikiana na serikali ya Malawi na wadau wa misaada ya kibinadamu, linahaha kuwanusuru zaidi ya watu 100,000 waliopoteza makazi kufuatia mafuriko nchini humo. Idadi hiyo inatarajiwa kuongezeka kutokana na mvua zinazotarajiwa kunyesha zaidi nchini humo ambapo maeneo yaliotahiriwa zaidi ni wilaya za Chikwawa and Nsanje.

Elizabeth Byrs ni msemaji wa WFP mjini Geneva

(SAUTI YA BYRS)

"Tutasafirisha zaidi ya tani mia za migawo ya vyakula vya dharura kwa njia ya ndege. Itasaidia kwa mahitaji ya sasa hivi ya chakula. Inabidi tupeleke vyakula vinavyoweza kuliwa papo hapo kwa sababu watu wengi hawana tena jinsi ya kupika. Mvua zimezidi kwa asilimia 400 wastani ya mvua za kawaida. Hali siyo ya kawaida. Ndio maana mashirika ya Umoja wa Mataifa yameshikamana ili kusaidia serikali ya Malawi."