Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kumbukizi ya majanga hutupatia stadi za kujiimarisha: Wahlström

Kumbukizi ya majanga hutupatia stadi za kujiimarisha: Wahlström

Mkuu wa Ofisi ya Umoja wa Mataifa inayohusika na upunguzaji wa athari za majanga UNISDR, Margareta Wahlström, amesema kumbukumbu ya majanga yaliyopita ni muhimu katika udhibiti wa athari zitokanazo na matukio hayo.

Amesema hayo katika taarifa yake wakati huu ambapo Japan inafanya kumbukizi ya miaka 20 tangu tetemeko kubwa la ardhi la Hanshin huko Kobe jimbo la Hyogo, lililosababisha vifo vya watu zaidi ya 6,400.

Bi. Wahlström ambaye atashiriki kumbukizi hiyo huko Japan, amesifu nchi hiyo kwa jinsi inavyotambua tukio hilo akisema inasaidia kuweka mikakati stahili ya kukabili zahma za aina hiyo akisema katika miaka 100 iliyopita, matetemeko ya ardhi makubwa zaidi ni matano na yametokea ndani ya miaka 10 iliyopita.

Amesema matetekeno hayo ikiwemo lile la Haiti yametoa mafunzo makubwa juu ya matumizi ya ardhi na ujenzi mijini kama njia ya kupunguza athari za majanga.