Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Palestina yalitaka Baraza la Usalama litekeleze wajibu wake

Palestina yalitaka Baraza la Usalama litekeleze wajibu wake

Mwakilishi wa Kudumu wa Palestina kwenye Umoja wa Mataifa, Riÿad Mansour, leo ameelezea masikitiko yake kwa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu kushindwa kwa Baraza hilo kutekeleza wajibu wake kuhusu suala la Palestina, kushindwa kuchangia juhudi za kupatia suluhu mzozo kati ya Israel na Palestina, pamoja na kuweka barabara ya kuaminika ya kupata amani.

Akizungumza kwenye kikao cha Baraza hilo leo kuhusu hali Mashariki ya Kati na suala la Palestina, Balozi Mansour amesema, Baraza la Usalama limeshindwa kuchukua hatua mathubuti kupata mwarubaine wa mzozo wa Israel na Palestina, hata ingawa imesadikiwa na wote kuwa hali hiyo siyo endelevu, na kwamba inatishia amani na usalama Mashariki ya Kati na kote duniani.

Mswada wa azimio uliowasilishwa na Jordan kwa niaba ya nchi za Kiarabu kwa Baraza la Usalama, ulikwenda sambamba na maombi yaliyofanywa katika maazimio ya awali . Maazimio hayo yanaendelea kukiukwa na Israel, taifa koloni, na Baraza hili linaendelea kuruhusu hilo kufanyika bila kufanya chochote. Ingawa mswada wa azimio hilo ulipingwa vikali, ukweli ni kwamba, yaliyomo yalikuwa muhimu kwa kufikia amani yenye haki, na yameungwa mkono na jamii ya kimataifa kwa miongo mingi.”

Mwakilishi huyo wa Palestina amehoji ni jinsi gani wanaweza kukoma kufanya maombi yao kwa Baraza la Usalama, huku Israel ikiendelea kukali ardhi yao na kuendeleza matatizo na mateso kwa wanadamu.

“Tutaacha vipi kufanya maombi yetu kwa jamii ya kimataifa wakati watu wetu wanaendelea kunyimwa uhuru wao, kunyanyaswa na ukukwaji haki huu ukiendelea? Tunapoketi kwenye chumba hiki, hali inazorota na kuwa mbaya zaidi kila siku, huku suluhu la amani likiendelea kutoweka kwa sababu ya Israel kukosa utashi wa kisiasa, ikiendeleza shughuli zake bila kutowajibika?”