Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ofisi ya haki za binadamu ya UM kufunguliwa Honduras

Ofisi ya haki za binadamu ya UM kufunguliwa Honduras

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ambaye yuko ziarani nchini Honduras amekuwa na mazungumzo na Rais wa nchi hiyo Juan Orlando Hernández mjini Tegucigalpa.

Wawili hao wamejadili masuala ya kiuchumi na kijamii nchini Honduras, hususan mpango wa serikali wa maisha bora kwa wote na uhusiano wake na ajenda ya kimataifa ya maendeleo endelevu baada ya mwaka 2015.

Halikadhalika Ban na rais Hernández wamejadili  hali ya usalama na haki za binadamu Honduras pamoja na umuhimu wa kujikita katika kuchangia siyo tu masuala ya maendeleo bali pia mabadiliko ya tabianchi.

Katibu Mkuu ameunga mkono nia ya serikali ya Honduras ya kuimarisha uhusiano wake na Umoja wa Mataifa kwa njia ya kufungua ofisi ya kamishna wa haki za binadamu nchini humo.