Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Miaka mitano baada ya tetemeko la ardhi, MINUSTAH inaendelea kusaidia Haiti kujijenga upya

Miaka mitano baada ya tetemeko la ardhi, MINUSTAH inaendelea kusaidia Haiti kujijenga upya

Wakati Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Haiti, MINUSTAH, umekumbuka waliokufa katika tetemeko la ardhi lililoua zaidi ya watu 200,000 tarehe 12, Januari, mwaka 2010, nchini Haiti bado changamoto zinazokumba nchi hii ni nyingi.

Katika mahojiano na Priscilla Lecomte wa Redio ya Umoja wa Mataifa, Walter Mulondi kutoka Radio ya MINUSTAH anazungumzia masuala ya watu ambao bado wanaishi kwenye kambi za wakimbizi wakikosa huduma za msingi na wakilalamikia serikali iwape mahali pa kujenga nyumba zao. Hapa Mulondi anaanza kwa kuelezea kilichofanyika katika kumbukizi.