Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja utatukwamua kwenye changamoto: Ban

Umoja utatukwamua kwenye changamoto: Ban

Katibu Mkuu wa  Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema zama za sasa zinakabiliwa na changamoto kubwa ikiwemo ugaidi, ukosefu wa usalama, umaskini wa kupindukia, njaa na mabadiliko ya tabianchi.

Akihutubia baraza la India linalohusika na masuala ya kigeni mjini New Delhi, Ban ametolea mfano mitandao ya kigaidi akisema inaeneza hofu na ukosefu wa utulivu kote duniani akisema kuna ukosefu wa kustahimiliana kidini, kirangi na hata kikabilia. Katibu Mkuu amesema hayo yote yanaweza kupatiwa suluhu kupitia..

“Binadamu wanaweza kukabiliana na changamoto hizo kwa kushirikiana kwa maslahi ya wote kwani ushirikiano hubadili nguvu ya mtu mmoja kuwa nguvu ya wote. Jukumu hili si mzigo bali ni fursa ya kipekee.”

Katibu Mkuu akagusia pia ukatili wa kijinsia nchini India ikiwemo ubakaji na ukatili wa kingono akisema hiyo ni changamoto maalum kwa nchi hiyo akisema hakuna nchi inayoweza kusonga mbele iwapo wanawake wanakwamishwa.

Amesema Umoja wa Mataifa utafanya kila uwezako kusaidia serikali ya India katika kuzuia ghasia dhidi ya wanawake, ukatili na hata kuhakikisha wale wanaofanya vitendo hivyo wanaadhibiwa.