Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Haki za walemavu wa ngozi,albino

Haki za walemavu wa ngozi,albino

Wiki hii wakuu mbalimbali wa Umoja wa Mataifa wamefanya ziara nchini Tanzania kutathimini hali ya haki za makundi mbalimbali ikwamo, mauaji ya vikongwe, ndoa za utotoni na  walemavu wa ngozi, albino. Viongozi hao wakiongozwa na maratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini humo Alvaro Rodrigue wamefanya ziara katika kanda ya ziwa kunakotajwa kushamiri kwa matukio ya mauaji ya walemavu wa ngozi. Ziara hii inafanyika wakati huu ambapo ni hivi karibuni mkoani Mwanza mtoto mwenye umri wa miaka minne Upendo Emmanuel, mwenye ulemavu wa ngozi kutekwa na watu wasiojulikana na hadi sasa hajapatikana. Hii ni sehemu ya matukio mfululizo ya adha wanazokutana nazo walemavu wa ngozi ikiwamo kukatwa viungo kwa imani za kishirikina na hvyo kusababisha vifo kama sio ulemavu wa maisha.

Akiwa mkoani Mwanza mwakilishi mkazi wa Umoja wa Mataifa Tanzania Alvaro Rodrigue ameitolea wito serikali ya nchi hiyo.