Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Leone akutana na wadau Libya ili kupiga jeki mazungumzo ya amani haraka

Leone akutana na wadau Libya ili kupiga jeki mazungumzo ya amani haraka

Katika jitihada za kutatua mgogoro wa kisiasa na usalama nchini Libya, Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu nchini humo, Bernardino Leon, amefanya mazungumzo na wadau  kuhusu njia za kukomesha uhasama na kuanzisha mazungumzo ya kisiasa.

Bw Leon amekutana mjini Tobruk na Tripoli na wadau wakuu ambao wanatarajiwa kushiriki katika mazungumzo yaliyopendekezwa,  na kusisitiza kwao haja ya kuitisha duru ya pili ya mazungumzo ya kisiasa haraka iwezekanavyo  kwa lengo la kuzuia nchi hiyo kutumbukia katika vita zaidi na kuanguka kwa uchumi.

Halikadhalika, Bw Leon amesema wengi wa raia wa Libya wanataka amani na kwa hiyo hawapaswi kuwekwa mateka na watu wachache wanaona kwamba wataweza kushinda mgogoro unaoendelea kwa njia ya kijeshi.

Aidha, Mjumbe huo amesema ni muhimu mjadala kati ya vyama vyote nchini Libya uanze hivi karibuni.