Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mamia ya Raia wauwa Sudan Kusini: UNMISS

Mamia ya Raia wauwa Sudan Kusini: UNMISS

Kitengo cha haki za binadamu cha Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Sudan Kusini, UNMISS kimetoa ripoti ya kurusa 33 ambayo inaonyesha madai kuwa vikosi vya upinzani vyenye silaha viliwaua mamia ya raia tarehe 15 Aprili 2014 baada ya kuchukua udhibiti wa Mji Mkuu wa Jimbo la Unity, Bentiu kutoka jeshi la serikali.Taarifa Kamili na Abdullahi Boru.

(Taarifa ya Abdullahi)

Ripoti hiyo inaelezea mauaji kadhaa ya watu na kundi lenye silaha ambalo lilishambulia  kituo cha ulinzi wa raia ya ujumbe wa kulinda amani nchini humo kilichoko nje ya Jonglei, mji mkuu wa jimbo la Bor siku mbili baadaye

Kwa mujibu wa ushahidi uliokusanywa na  kuchambuliwa pamoja na mahojiano na watu 142, Ripoti inadhibitisha kuna sababu za msingi za kuamini kwamba kwa uchache raia 353 waliuawa na wengine  250 kujeruhiwa katika mashambulizi.

Rupert Colville ni msemaji wa Ofisi ya Haki za Binadamu

(SAUTI Rupert Colville)

"Kwenye tukio la kwanza Bentiu, tarehe 15, Aprili, takbribani raia 287 wameuawa kwenye msikiti na waasi baada ya kuchukua upya mji mkuu wa jimbo la Unity. Wengi wao walikuwa wafanyabiashara wa Sudan na familia zao ambao wameuawa kwa msingi wa kabila lao la kidarfur.  Na kiasi cha 19 wameuawa siku hiyo hiyo katika hospitali ya Bentiu."