Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu ya wakimbizi wakimbia mashambulizi Kaskazini Mashariki mwa Nigeria

Maelfu ya wakimbizi wakimbia mashambulizi Kaskazini Mashariki mwa Nigeria

Wakimbizi zaidi ya elfu saba kutoka Nigeria wamewasili Magharibi mwa Chad kwa muda wa siku kumi zilizopita wakikimbia mashambulizi mjini Baga na vitongoji vyake huko kaskazini mashariki mwa Nigeria, kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuwahudumia wakimbizi duniani UNHCR .Taarifa kamili na Grace Kaneiya(Taarifa ya Grace)

Kulingana na vyombo vya habari ripoti zinasema kwamba mashambulizi mjini Baga yalisababisha vifo vya  mamia ya watu huku wengi wakikimbia makwao. Wengi wa wakimbizi wanahifadhiwa na jamii katika vijiji mbali mbali, ambako Serikali ya Chad imeomba msaada. Adrian Edwards ni msemaji wa UNHCR mjini Geneva.

Mamlaka nchini Chad walitembelea eneo hilo na kuomba msaada kwa UNHCR wa kuwahamisha Zaidi ya wakimbizi elfu moja ambao wanadaiwa kukwama katika kisiwa cha Kangala katika Ziwa Chad.Watu hao wamewasili baada ya kukimbia mzozo Kaskazini mashariki mwa Nigeria, kwa sasa Chad inahifadhi takriban wakimbizi elfu kumi.”

UNHCR tayari imeanza kutoa misaada ya vyandarua, mitungi ya kubebea maji, mikeka, mablanketi na vifaa vya jikoni kwa ushirikano na wadau.