Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama labariki MONUSCO na FARDC kuiadabisha FDLR

Baraza la usalama labariki MONUSCO na FARDC kuiadabisha FDLR

Baraza la usalama leo limekutana kujadili hali nchini jamhuri ya kidemokrasia ya kongo DRC ambapo baraza hilo limeezea kusikitishwa kwake na hali ya usalama na kibinadamu nchini humo hususani mashariki mwa nchi.

Rais wa baraza hilo kwa mwezi huu kutoka Chile Cristian Barroso ameliambia baraza hilo kuwa baraza linafahamu tarehe ya mwisho ikliyowekwa na mkutano mkuu wa maziwa makuu (ICGLR) na jumuiya ya uchumi kusini mwa Afrika (SADC) kwa makundi yenye silaha kujisalimisha imepita bila makundi hayo kufanya hivyo ikiwamo waasi wa FDLR.

Kufuatia hilo baraza limesisitiza umuhimu wa jeshila la DRC na kikosi cha ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO kutekeleza mpango wa kutumia nguvu za kijeshi dhidi ya FDRL ili kudhoofisha kundi hilo.

Awali baraza la usalama lilisimama kwa muda mfupi kuomboleza vifo vya watu kumi na mbili wakiwamo wachora vibonzo wa gazeti nchini Ufaransa liitwalo Charlie Hebdo.