Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

MONUSCO haiwezi kuondoka DRC nchi ikiwa bado dhaifu: Kobler

MONUSCO haiwezi kuondoka DRC nchi ikiwa bado dhaifu: Kobler

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, ambapo, Mkuu wa Ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO, Martin Kobler amewaeleza waandishi wa habari maswali yatakayopewa kipaumbele na ujumbe huo mwaka 2015. Taarifa zaidi na Amina Hassan.

(Taarifa ya Amina)

Lengo la kwanza la MONUSCO mwaka huu ni operesheni za kijeshi dhidi ya kundi la waasi wa FDLR, Martin Kobler amesema kwamba , licha ya juhudi za jamii ya kimataifa na serikali ya DRC, wameshindwa kusalimisha kundi hilo kwa amani

“ Utaratibu huo haukuwezekana, haukuwa na ukweli. Tumetumia dola milioni 1.6 kwa ajili ya kambi za kusamilisha FDLR Kisangani, Kanyabayonga na Walungu lakini ni waasi 357 tu waliopatikana.”

Aidha Mwakilishi huyo Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema MONUSCO inazingatia umuhimu wa kusaidia maendeleo ya kiuchumi katika maeneo yaliyopata amani mashariki mwa DRC nakuongeza kuwa itaweka kipaumbele katika uboreshaji wa mamlaka za kitaifa kama ilivyokubaliwa katika makubaliano ya Addis-Abeba, ikiwa ni

Maridhiano ya kitaifa, mwelekeo wa kisiasa, uchaguzi, kwa sababu MONUSCO hauko hapa kwa milele. Lakini hatuwezi kuondoka nchi ikiwa bado dhaifu.

(Sauti kutoka kwa Radio Okapi)