Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa waliofia kazini wakumbukwa

Wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa waliofia kazini wakumbukwa

Hapa katika Umoja wa Mataifa hii leo kumefanyika kumbukumbu maalum ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa waliopoteza maisha wakati wakitumikia Umoja huo. Grace Kaneiya amefuatilia tukio hilo.

(TAARIFA YA GRACE)

Ni kifaa maalum cha muziki aina ya Fidla kikipigwa ikiwa ni sehemu ya kumbukizi ya wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa waliopoteza maisha yao wakati wakiwa katika majukumu ya kulinda Amani, kutetea haki za binadamu na maendeleo.

Tukio hili pia limetumika kuwakumbuka wafanyakazi zaidi ya 100 waliokufa wakati wa tetemeko la ardhi nchini Haiti miaka mitano iliyopita.

Katibu mkuu Ban Ki-moon akasema kile kinachofanywa na Umoja huo katika usalama wa wafanyakazi.

"Tumejidhatiti kwa uthabiti kuhusu usalama wa wafanyakazi wetu na tunajaribu kutafuta njia mpya za kukuza usalama na kupunguza majanga. Vifaa bora na mafunzo ni sehemu ya suluhisho. Tunaomba nchi wanachama kuunga mkono juhudi hizi kifehda, na kuhakikisha kuwa wale wanaoshambulia wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanafikishwa katika mkono wa sheria."

Mmoja wa manusura wa tetemeko la ardhi huko Haiti akaibua hisia za majonzi.

(SAUTI)

Miongoni mwa wafanyakazi waliokumbukwa katika hafla ya leo ni 100 waliofariki waliofariki kati ya Oktoba 2013 hadi Novemba 2014.