Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mauaji katika gazeti nchini Ufaransa ni shambulizi dhidi ya demokrasia : Ban

Mauaji katika gazeti nchini Ufaransa ni shambulizi dhidi ya demokrasia : Ban

Shambulizi dhidi ya gazeti l a kukejeli liitwalo Charlie Hebdo, mjini Paris, Ufaransa, ambapo watu 12 wameripotiwa kufariki dunia, linaathiri moja kwa moja misingi ya demokrasia, kwa mujibu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon.

Watu watatu wanaoshukiwa kuwa wafuasi wa kundi la kigaidi la Al-Qaida wamevamia ofisi za Charlie Hebdo jumatano hii na kuwapiga risasi waandishi wa habari na wachoraji vibonzo, pamoja na askari wa polisi.

Alipozungumza wakati wa mkutano wa mwaka wa waandishi mjini New York, Ban Ki-moon amesema

"Nataka kueleza kushtushwa sana na shambulizi hilo la kudharaulika sana dhidi ya gazeti ya kifaransa ya Charlie Hebdo. Mauaji hayo yalikuwa ya kutisha, na hayathibitishwi. Pia ilikuwa ni shambulizi ya moja kwa moja dhidi ya msingi moja wa demokrasia, yaani vyombo vya habari na uhuru wa kujieleza”

Gazeti hilo limejulikana kwa kutoa vibonzo kuhusu dini ya kiislamu na waandishi wake waliwahi kutishiwa kwa sababu hiyo. Mwaka 2011 tayari ofisi za gazeti hilo zilichomwa moto na watu waliodaiwa kuwa magaidi.

Aidha baraza la usalama limelaani vikali tukio hilo dhidi ya gazeti na waandishi wa habari, Wanachama wa baraza hilo wametuma rambirambi zao kwa familia za wahanga na serikali ya Ufaransa.