Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP yasaidia familia ziloathiriwa na ukame nchini Afghanistan

WFP yasaidia familia ziloathiriwa na ukame nchini Afghanistan

Shirika la mpango wa chakula duniani, WFP, kwa kushirikiana na serikali ya Australia a limeanza miradi wa kuboresha maisha na kupunguza athari za janga kwa jamii zinazoishi Tharparkar, Sanghar na Mirpurkhas wilayani Sindh nchini Afghanistan.

WFP inawezesha mpango huu kufuati ruzuku ya dola zaidi ya milioni 2 kutoka kwa serikali ya Australia. Mwakilishi na Mkurugenzi wa WFP nchini Afghanistan, Lola Castro amesema walengwa wa mradi huo ni familia zinazokabiliwa na ukame ambao amesema unaathiri maisha ya watu wanaoishi katika maeneo hayo , kwa hiyo mradi huu utaziwezesha jamii kujenga vitu vitakavyozisaidia jamii kuboresha maisha na usalama endelevu wa chakula.

Familia 13,200 zitapokea malipo ya fedha kwa ajili ya kushiriki shughuli za kupunguza maafa hatari.