FDLR lazima isitishe operesheni zake DRC : MONUSCO

FDLR lazima isitishe operesheni zake DRC : MONUSCO

Lazima kundi la waasi wa FDLR lisistishe operesheni zake Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC kwa amani ili kuleta utulivu nchini humo amesema  Kamanda Mkuu wa vikosi vya ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini  DRC MONUSCO, Jenerali Carlos Alberto dos Santos Cruz. Taarifa zaidi na Joseph Msami.

(Taarifa ya Msami)

Katika mahojiano na radio ya Umoja wa Mataifa kutoka DRC Jenerali Cruz amesema licha ya kwamba muda uliokuwa umewekwa kwa kundi hili kujisalimisha kwa hiari Janury 2 mwezi huu umepita, mustakabali wa amani na utulivu unategemea kundi hili kujisalimisha.

(SAUTI CRUZ)

"Ni muhimu sana FDLR kusitisha shughuli zake Mashariki mwa Kongo kuleta utulivu zaidi. Ni muhimu kisiasa pia. MONUSCO na jeshila taifa tunafanya kazi vyema katika operesheni na tuna mpango wa pamoja."

Hata hivyo amesema MONUSCO ina matarajaio kuwa  viongozi wa FDLR watatekeleza makubaliano.

(SAITI CRUZ)

"Natarajia kuwa viongozi wa FDLR wana jukumu la kujisalimisha kutoakana na mazungumzo na makubaliano waliyofanya na ajumuiya ya kimataifa".