Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ripoti Mpya ya UNHCR inaonyesha kuongeza kwa watu waliofurushwa makwao 2014

Ripoti Mpya ya UNHCR inaonyesha kuongeza kwa watu waliofurushwa makwao 2014

Ripoti mpya ya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Wakimbizi, UNHCR inasema kuwa mapiganano yanayoendelea katika sehemu kubwa ya Mashariki ya Kati, Afrika na maeneo mengine duniani yamechangia kwa wastani kwa watu zadi ya milioni 5 kukimbia makwao katika nusu ya mwaka wa 2014. Taarifa kamili na Abdullahi Boru.

(Taaarifa ya Abdullahi)

Repoti hiyo mpya ya UNHCR inaonyesha  kuwa watu milioni 5.5 wapya wamekimbia makwao, kati ya hao watu milioni 1.4 wakivuka mipaka ya kimataifa na kwa hivyo kuwa wakimbizi, huku wengine wakisalia kuwa wakimbizi wa ndani katika nchi zao.

UNHCR imesema kwa  kuzingatia watu waliofurushwa tayari, marekebisho ya taarifa, watu waliorudi makwao kwa hiari na waliopata makazi, idadi ya watu waliosaidiwa na shirika la UNHCR imefikia watu milioni 46.3 kufikia kati kati ya mwaka wa 2014, ikiwa ni nyongeza ya watu milioni 3.4 kuliko mwaka jana, na idadi hiyo ni rekodi mpya ya juu.

Adrian Edwards ni Msemaji wa UNHCR

“Mgogoro wa Syria ndio umebadili kila kitu. Kufikia kati kati ya mwaka wa 2014, kumekuwa na wakimbizi na watu waliofurushwa makwao milioni 10. Kwa sasa Wasyria wamekuwa kundi kubwa la wakimbizi duniani. Kwani kati ya watu wanne ambao ni wakimbizi, mmoja wao anatoka Syria”

Barani Afrika, mataifa mengine ambapo kuna wakimbizi  ni pamoja na Kenya, Ethiopia, na Chad.