Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Umoja wa Mataifa walaani shambulizi dhidi ya gazeti ya Charlie Hebdo Ufaransa

Umoja wa Mataifa walaani shambulizi dhidi ya gazeti ya Charlie Hebdo Ufaransa

Tuanzie Ufaransa, msikilizaji, ambapo Umoja wa Mataifa umelaani shambulizi lililowalenga waandishi wa habari na polisi kusababaisha vifo vya watu 12 na wengine 20 kujeruhiwa katika shambulizi lililotajwa kuwa la kigaidi dhidi ya gazeti linaloandika habari za  kukejeli, mjini Paris Ufaransa . Taarifa zaidi na Priscilla Lecomte.

(Taarifa ya Priscilla)

Kamisha Mkuu wa haki za binadamu Zeid Ra'ad Al Hussein amelaani vikali tukio hilo dhidi ya gazeti liitwalo Charlie Hebdo katika taarifa iliyotolewa na ofisi yake.

Amesema uhuru wa kujieleza na kutoa maoni ni msingi wa kila demokrasia, na wale ambao wanajaribu kutengana jamii kwa misingi ya dini au kabila hawapaswi kufanikiwa.

Ametuma rambirambi zake kwa familia za wahanga na kuwatakia nafuu waliojeruhiwa.

Zeid ameongeza pia kwamba anahofia tukio hilo litatumiwa na watu wenye msimamo mkali wa ubaguzi dhidi ya wahamiaji.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la elimu , sayansi na utamaduni UNESCO , Irina Bokova ameeleza kushtushwa sana na shambulio hilo akisisitiza kwamba UNESCO utaendelea kupigania uhuru wa magazeti.